Huduma za Lugha ya Kiswahili

Waarabu wa Pemba huelewana kwa vilemba. (Methali)

Kiswahili ni lugha ya mawasiliano inayotumika na watu zaidi ya milioni 80 katika Afrika ya Mashariki. Kwa hivyo, lugha hii inazidi kuwa na umuhimu ulimwenguni kote.

Tunatoa huduma za lugha ya Kiswahili zifuatazo:

Utafsiri
Tunatoa huduma za kutafsiri maandiko mbalimbali, kwa mfano: barua, mikataba, tovuti, baruapepe, vijitabu n.k. kutoka Kiswahili hadi Kijerumani au Kiingereza na pia kutoka Kijerumani au Kiingereza hadi Kiswahili katika fani zifuatazo, miongoni mwa zingine:

- Mawasiliano ya kawaida
- Sheria
- Utamaduni
- Uchumi/Biashara
- Udaktari
- Dini
- Sayansi
- Uhandisi/Tekniki

Kwa kuwa tuna tajriba za miaka mingi, kazi ya utafsiri itakamilishwa bila kuchelewa na itakuwa na usahihi na ubora zaidi.

Ustadi wa lugha
Kwa kushirikiana na wazungumzaji wazawa wa Kiswahili pamoja na wataalamu wa lugha ya Kiswahili kutoka Afrika ya Mashariki tunawahakikishia wateja wetu usahihi na ubora wa kazi yetu kila wakati.

Ukalimani
Ikiwa unapanga kuzuru Ulaya, iwe kikazi, kibiashara au kibinafsi, na unahitaji mkalimani, nitakuwa tayari kukusindikiza wakati wa ziara zako. Vilevile nitakuwa tayari kuwasindikiza wageni wenu kutoka Ulaya wakizuru Afrika ya Mashariki.

Wasiliana nasi: swahili(at)ostafrika-service.de